HATIMAYE usiku wa tuzo za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 umegota mwisho na kila kitu kuwa wazi nani amekuwa nani baada ya tuzo hizo.
Kwenye kikosi bora cha msimu nyota wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi wametawala kila kona huku kwa upande wa Simba ambao ni watani zao wa jadi mchezaji mmoja pekee akipenya kwenye kikosi cha kwanza.
Hiki hapa kikosi bora kipo namna hii:-
Ley Matampi wa Coastal Union
Yao Kouassi wa Yanga
Mohamed Hussen wa Simba
Ibrahim Hamad wa Yanga
Dickson Job wa Yanga
Mudathir Yahya wa Yanga
Kipre Junior wa Azam FC
Maxi Nzengeli wa Yanga
Wazir Junior wa KMC
Feisal Salum wa Azam FC
Aziz Ki wa Yanga