SUPU YANGA YAKUTOSHA KUTOKA SPORTPESA

UHAKIKA kuelekea kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi kutakuwa na supu ya maana kutoka kwa SportPesa wadhamini wakuu wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Yanga Agosti 4 inatarajiwa kuwa ni kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo ni siku maalumu ya utambulisho kwa benchi la ufundi la Yang, wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi hicho msimu wa 2023/24.

Miongoni mwa wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Yanga ni pamoja na Bacca, Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Nondo, Sure Boy, Jonas Mkude huku wapya ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Prince Dube, Duke Abuya.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya ameweka wazi kuwa wameandaa supu ya uhakika kwa wananchi ikiwa ni maalumu kwa ajili wale wote watakaojitokeza Jumamosi.

“Sisi kama wadhamini wakuu tutakuwa pamoja kwenye supu day siku ya jumamosi, Kampuni ya Sportpesa imeandaa supu kwa wananchi wakiwa wanajiandaa kupata burudani kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi.”

Mbali na supu pia kutakuwa na zawadi kwa mashabiki ikiwa ni kampeni maalumu iliyoandaliwa na SportPesa ambapo Tracy Humplick Meneja Masoko wa SportPesa Tanzania amesema: “Tumeandaa Kampeni maalumu kwa mashabiki wote wa Yanga Sc, tutakuwa tunagawa jezi mpya za msimu huu kama zawadi kwa mashabiki wa Yanga Sc kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi.”