YANGA KUCHEZA DHIDI YA RED ARROWS KWENYE KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI – VIDEO

Klabu ya Yanga kupitia kwa Msemaji wake, Haji Manara imetangaza kuwa watacheza dhidi ya Mabingwa wa Michuano ya KAGAME Cup, Red Arrows kutoka Zambia kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi kitakachofanyika August 04,2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Champion wa Kagame Cup msimu huu, Red Arrows kutoka Zambia ndio timu tutakayocheza nayo siku ya Tarehe 4, pale Benjamin Mkapa Stadium na wametuambia watakuja na Ndege yao ya Jeshi,” ——Msemaji wa Yanga Sc, Haji Manara.