UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa itakuwa ni ubaya ubwela Agosti 3 2024 kutokana na mpango kazi uliopo ndani ya timu kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Simba Day linalotarajiwa kuwa na mwendelezo wa mvuto Uwanja wa Mkapa.
Tayari Simba wamezindua uzi mpya wa msimu wa 2024/24 ilikuwa ni Julai 24 Morogoro na Sandaland anahusika kwenye usambazi wa uzi mpya ambao kwa sasa unapatikana kila kona ya Tanzania.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa ni siku kubwa kwa mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa ili kuona burudani, wachezaji watakaopeperusha bendera kitaifa na kimataifa.
“Siku kubwa inakuja na maandalizi yapo vizuri. Ubaya ubwela itakuwa kwani kuna wachezaji wa ubaya ubwela, mashabiki wa ubaya ubwela kila kitu kitakuwa kwenye mpangilio mzuri na furaha itakuwa kubwa kwa kila atakayekuja Uwanja wa Mkapa.
“Tumeshakamilisha uzinduzi wa uzi mpya, matirio yake hayajawahi kutumika kutokana na uimara wake hivyo mashabiki ni muda wa kununua uzi mpya na kutamba nao kwa kuwa ni mzuri vibaya mnoo.”