>

UBAYA UBWELA NOMA SANA KUIBUKA KWA MKAPA

WAKATI uzi mpya wa Simba uliozinduliwa Julai 24 ukizidi kuwa gumzo kila kona kutokana na ubunifu wake pamoja na nembo ambazo zimetumika uongozi wa timu hiyo umebainisha kuwa ubaya ubwela hautaishia kwenye uzi pekee bali mpaka mechi zao zote kazi ipo palepale.

Miongoni mwa mechi ambazo zinasubiriwa kwa shauku kubwa kwa sasa ni Kariakoo Dabi kati ya Simba dhidi ya Yanga itakuwa ni Agosti 8 Uwanja wa Mkapa ambapo itakuwa ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa kurejea kwa ligi inayotarajiwa kuanza Agosti 16 2024.

Ni Simba walitwaa taji la Ngao 2023/24 wana kibarua cha kutetea taji hilo mbele ya Yanga iliyotwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita ikikamilisha mzunguko wa pili na pointi 80 kibindoni.

Agosti 3 2024 itakuwa ni Simba Day ambapo wachezaji wapya na waliokuwa na kikosi msimu uliopita watatambulishwa rasmi kwa mashabiki na dunia kiujumla huku King Kiba akitajwa kuwa atatoa burudani siku hiyo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wataendelea na ubaya ubwela mpaka Agosti 8 katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii.

“Ubaya ubwela utaendelea na tumeona kwamba Agosti 8 tutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii basi tunafanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu muhimu Uwanja wa Mkapa. Mashabiki mjitokeze kwa wingi kuwashangilia wachezaji wetu ili kuwaongezea nguvu kuendelea kuwapa burudani uwanjani.”