>

AZAM FC YAMUONGEZEA MKATABA KIUNGO WA KAZI

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo wa kazi Tepsi Evance ambaye ni moja ya wazawa wenye vipaji vikubwa kwenye kucheza na mpira.

Tepsi ambaye alikuwa kwa mkopo ndani ya KMC msimu wa 2023/24 bado atabaki kuwa mali ya Azam FC mpaka 2026 baada ya kuogeza kandarasi ya mwaka mmoja.

Kiungo huyo amebainisha kuwa ni furaha kwake kuongeza mkataba kuwa ndani ya Azam FC hivyo atapambana kufanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wengine.

“Furaha yangu kuendelea kuwa ndani ya Azam FC nipo tayari kwa ajili ya kupambana ili kufanya vizuri kwa timu ya Azam FC nina amini inawezekana.”

Azam FC imeweka kambi Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 16 2024. Ngao ya Jamii inatarajiwa kuwa Agosti 8 2024 ambapo Azam FC watacheza nusu fainali dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa New Amaan Complex.