>

FAINALI YA CECAFA INAPIGWA LEO, APR V RED ARROWS

INAITWA Armée Patriotique Rwandaise Football Club au APR kama wengi ambavyo wamezoea ilianzishwa 1993 June Mosi. Licha ya historia yao fupi, wamekuwa mojawapo ya klabu zilizofanikiwa zaidi katika ligi ya Rwanda wakishinda mataji ishirini na mawili ya ligi ya Rwanda na makombe kumi na tatu ya Rwanda Cup.

APR FC pia imeshinda makombe matatu ya CECAFA Kagame Cup ikiwa ni mwaka 2004, 2007 na 2010 huku ikipoteza fainali mbili katika mashindano haya ambapo ni 1996 na 2000. Ina kazi nyingine leo kwenye mchezo wa fainaliinayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

 2022 ilifika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa ya CAF kwa mara ya kwanza katika historia ya vilabu. Hii leo wapo dimbani tena katika fainali ya CECAFA Kagame Cup ambapo wanakwenda kuvaana na Red Arrows kutoka nchini Zambia.

Licha ya APR kuwa na nguvu katika kujilinda wameonyesha pia hawana makali kwenye kufunga kwani wamefunga mabao matatu pekee hadi fainali. Kuingia fainali, timu ya Rwanda ilizisimamisha Singida Black Stars (Tanzania) na El Merriekh Bentiu (Sudan Kusini) kwa bao 1-0, na kutoka sare ya 1-1 na SC Villa ya Uganda katika mechi ya mwisho ya kundi. Waliendelea kwa kuwatoa Al Hilal kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kuisha bila bao katika hatua ya nusu fainali.

Kwa Red Arrows FC watakuwa timu ya kutazama kuelekea fainali. Kocha Chisi Mbewe alianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Gor Mahia FC (Kenya), lakini akapokea kichapo kikubwa cha 5-0 kutoka kwa Al Hilal katika mechi ya pili. Katika mechi ya mwisho ya do-or-die walifanikiwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya ASAS Djibouti Telecom. Katika hatua ya nusu fainali walifunga mabao mawili katika kipindi cha pili cha muda wa nyongeza baada ya mechi kumalizika bila bao katika dakika 90.

Ameandika Cosmas Choga