YANGA KUMALIZANA NA MSHAMBULIAJI HUYU

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kuna wachezaji ambao watatambulishwa ndani ya kikosi hicho wakiwa na uwezo mkubwa jambo litakaloongeza nguvu kuelekea msimu wa 2024/25.

Yanga inanolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi msimu wa 2023/24 safu ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 71 na kinara alikuwa ni Aziz Ki aliyefunga mabao 21.

Kwa upande wa maingizo mapya kwenye ushambuliaji ni Prince Dube ametambulishwa kuwa ndani ya kikosi cha Yanga anaungana na Clement Mzize, Kennedy Musonda.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanafanya maboresho kwenye kikosi hicho ili kuwa imara kwa ajili ya mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

“Kazi kubwa inafanyika kwenye upande wa maboresho ya kikosi ambapo katika kila idara tunafanya maboresho kuwa imara na bora. Kuna washambuliaji ambao wanakuja na tunatambua wakitambulishwa kuna watu watatetemeka kwa sasa.

“Yupo Prince Dube, Clement Mzize hivyo tunaamini kwamba washambuliaji wengine wanakuja ambao watakuwa na nguvu kwenye kutimiza majukumu yao.”

Miongoni mwa washambuliaji wanaotajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga ni Jean Baleke aliyewahi kucheza Simba msimu wa 2023/24 na alipokutana na Thank You alikuwa kafunga jumla ya mabao 8.