>

YANGA WAMTAMBULISHA MTAALAM WA TIBA YA VIUNGO

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/24 Yanga wanaendelea na mipango kazi ya maboresho ya kikosi kuelekea msimu wa mpya wa 2024/25.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilikamilisha mzunguko wa pili ikiwa na jumla ya pointi 80 baada ya kucheza mechi 30 ikipoteza michezo miwili pekee ugenini dhidi ya Ihefu na Azam FC kwenye Mzizima Dabi.

Katika mchezo wa mzunguko wa pili wakati ikifungwa na Azam FC ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Azam FC 2-1 Yanga, bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Fei Toto.

Julai 12 2024 Yanga ilimtambulisha mtu mwingine wa kazi kwenye sekta ya afya ambaye huyu ni mtaalamu kwenye masuala ya Tiba na Viungo.

Ni Sekhwela Seroto, Mtaalam wa Tiba ya Viungo (Physiotherapist) raia wa Afrika Kusini atakuwa ndani ya Yanga.