>

ANACHOMOLEWA MWINGINE KUTOKA UNYAMANI KUIBUKIA JANGWANI

WATOTO wa Jangwani, Yanga hawana jambo dogo ambapo inatajwa kuwa wapo kwenye hesabu za kumchomoa mwamba mwingine kutoka unyamani kwa ajili ya kuwa naye ndani ya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Tayari wanaye Clatous Chama ambaye ni kiungo mshambuliaji aliibuka hapo bure baada ya mkataba wake kugota mwisho.