MWAMBA KIBWANA SHOMARI BADO YUPO YANGA

BADO yupoyupo sana ndani ya kikosi cha Yanga mwamba Kibwana Shomari ambaye ni mzawa baada ya kuongeza kandarasi nyingine.

Yanga kupitia kwa Ofisa Habari Ali Kamwe walibainisha kwamba watafanya usajili bora utakaozingatia vigezo vya uwezo kwa wachezaji ili kuongeza ushindani ndani ya timu.

“Kila mchezaji ana nafasi ya kuonyesha uwezo wake na tunaamini kwenye ubora wao hivyo tutasajili wachezaji wazuri na wale ambao wapo ndani ya kikosi tutawaongezea mikataba.”

Kibwana ameongeza mkataba mpya utakaomfanya awe na uhakika wa kuwa kwenye kikosi hicho msimu wa 2024/25.

Ni mpaka 2026 nyota huyo aliyeibuka ndani ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro atakuwa hapo kutimiza majukumu yake.

Tayari mabingwa hao wa ligi msimu wa 2023/24 wameanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ukiweka kando Kibwana pia mwamba Farid Mussa naye ni miongoni mwa wachezaji ambao wameongeza mkataba ndani ya kikosi hicho cha Yanga.

Chini ya Miguel Gamondi, Yanga ilitwaa taji la ligi itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa ipo wazi kwamba 2023/24 iligotea hatua ya robo fainali