MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Yanga wameendelea na maboresho ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu,Miguel Gamondi kwa kumtambulisha kipa wa mpira kuwa ingizo jipya.
Ni kipa wa kazi Khomeiny Abubakary akitokea Ihefu atakuwa kwenye changamoto mpya ndani ya Yanga kwa msimu wa 2024/25 akitimiza majukumu yake.
Uwepo wake ndani ya Yanga utaongeza idadi ya makipa kuanzia yule namba moja Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery pamoja na makipa wa timu za vijana ambao wamekuwa wakiaminiwa kwa ajili ya kuandaliwa kuwa kwenye majukumu mapya wakati ujao.
Msimu uliopita rekodi kutoka Azam TV zinaonyesha kuwa alicheza mechi 14 akiwa na uzi wa Ihefu SC, akitumia dakika 1172 na kujikusanyia “clean sheet” nne (4) kwenye NBC Premier League.
Kwenye mchezo wa fainali ya CRDB Federatin Cup nyota kipa huyo alikuwa langoni na mwisho ni Yanga walitwaa taji hilo na mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa uligotea kwenye dakika 120.