>

YANGA YATANGAZA RASMI KUMUONGEZA MKATABA MSHERY

KLABU ya Yanga imetangaza rasmi kumuongeza mkataba wa mlinda mlango wao namba (2), Aboutwalib Mshery (23).

Mshery kwa msimu wa 2023/24 hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na kutokuwa fiti mwanzo wa msimu lakini mwisho wa msimu alikuwa akipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake.

Anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliocheza hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na kikosi cha Yanga ikiwa imepiteza zaidi ya miaka 19 kwa timu hiyo kucheza hatua hiyo.

Dili lake jipya ambalo ameliongeza ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi litamfanya awepo hapo mpaka 2027 akitimiza majukumu yake.

Anaendelea kusalia hapo ndani ya Yanga kwa ajili ya kupambania malengo yaliyopo ndani ya timu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya SportPesa.