>

SIMBA YATHIBITISHA KUKAMILISHA UHAMISHO WA KIUNGO DEBORA

Klabu ya Simba Sc imethibitisha kukamilisha uhamisho wa kiungo Debora Fernandes Mavambo (24) kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Mutondo Stars ya Zambia.

Debora ambaye ana uraia pacha wa Congo Brazaville lakini anachezea timu ya taifa ya Gabon anamudu pia kucheza kama kiungo mkabaji ingawa anapendelea zaidi kucheza kama kiungo wa kati (namba 8).