VIDEO: GERSON MSIGWA AFICHUA ZA NDANI KABISA – “RAIS SAMIA AMETOA MILIONI 100 KWA TAIFA STARS….

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa @gersonmsigwa amesema kama taarifa kwamba Ligi Kuu ya Tanzania imeshika nafasi ya tano kwa ubora Afrika ni uhakika, basi sio jambo dogo hata kidogo.

Msigwa amesema anawapongeza wanamichezo na wadau wote kwa jinsi walivyoweza kuiboresha ligi yetu na kuifanya kuwa ya ushindani mkubwa.

Ameyasema hayo kwenye Exclusive Interview aliyoifanya na Global TV ndani ya studio zake za kisasa zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.