>

TETESI: YANGA KUACHANA NA WACHEZAJI SITA

Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Nyota wake 6 ambao ni Mghana Agustine Okrah, kiungo Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Afrika Kusini, Mkongo Joyce Lomalisa, Zawadi Mauya, Metacha Mnata na Joseph Guede kutoka nchini Ivory Coast.

Taarifa za ndani zinasema tayari wa Uongozi wa Yanga SC wamemaliza kuwaongezea mikataba nyota wote watakaosalia kikosini hapo kwa msimu 2024-25 lakini majina va wachezaji hao sio sehemu ya wachezaji waliongezewa mikataba kuelekea msimu ujao wa Mashindano ndani ya Yanga SC.