MTAMBO WA MABAO WATAMBULISHWA SIMBA

WAKIWA kwenye maboresho ya kikosi kuelekea msimu wa 2024/25 wamemtambulisha nyota mwingine ambaye ni mtambo wa mabao.

Ni Simba iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo msimu wa 2023/24 kwa sasa inafanya maboresho ambapo kwenye eneo la kiungo ipo wazi haitakuwa na Clatous Chama ambaye kaibukia ndani ya Yanga.

Mchezaji mpya ambaye ametambulishwa Julai 5 ndani ya kikosi cha Simba ni kiungo mshambuliaji Valentino Mashaka.

Ikumbukwe kwamba  2023/24, Valentino Mashaka alitupia kambani jumla ya mabao sita na kutoa pasi moja ya bao akiwa na Geita Gold FC kwenye NBC Premier League.

Nyota alicheza mechi 24 za NBC Premier League akitumia dakika 1393 atakuwa ndani ya Simba SC kwa kandarasi ya miaka miwili.