LUIS MIQUISSONE AREJEA KWENYE KLABU YAKE YA ZAMANI YA UD DO SONGO

ALIYEKUWA winga wa Klabu ya Simba Luis Miquissone amerejea kwenye klabu yake ya zamani ya UD do Songo kwa ajili ya msimu ujao wa 2024/25.

Luis anatajwa kuwa alikuwa anakunja mkwanja mrefu ndani ya kikosi cha Simba akiwa anakula sahani moja na Aziz Ki kiungo wa Yanga kwenye upande wa kuvuta mkwanja mrefu Bongo.

Miquissone anarejea UD do Songo baada ya kuwa nje kwa miaka minne akiiwakilisha Simba ya Tanzania (2020 na 2023), El Ahly ya Misri (2021 na 2023) na Abha Club kutoka Saudi Arabia (2022).

Kabla ya kuondoka UD Songo, Miquissone ilishinda Kombe la Msumbiji mnamo 2016 na ubingwa wa kitaifa mnamo 2017.

Ipo wazi kuwa ndani ya Simba kwa msimu wa 2023/24 kiungo huyo alitoa jumla ya pasi tatu za mabao ndani ya ligi.

Hakuwa chaguo la kwanza kwa kocha Mkuu Juma Mgunda kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza jambo lililofanya kiwango chake kikaporomoka.