>

đ—Ļ𝗔𝗕𝗔𝗕𝗨 đ—Ŧ𝗔 𝗞𝗨𝗖𝗛𝗘𝗟𝗘đ—Ē𝗔 USAJILI WA BOKA YANGA

Wing-back fundi Chadrack Boka (24) @chadrac.boka ndiye mchezaji wa 1 kusajiliwa na Yanga SC 24|25.

Amesaini mkataba wa miaka miwili, kinachosubiriwa ni (ITC) yake pekee.

Amechelewa kuwasili Nchini Tanzania kwa sababu klabu aliyotoka FC Lupopo haikutaka mchezaji huyo aondoke.

FC Lupopo wanadai mchezaji huyo ni wao wamekiambia Chama cha soka Nchini DRC (FA) kisitume (ITC) kwenda Yanga SC kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Mchezaji na management yake wanapambana kutafuta (ITC) ili awahi kuripoti kambini Tanzania kuanzia July (8).

ℹī¸ Mchezaji huyo aliyefanya vizuri katika ligi kuu ya DR Congo sio mchezaji wa FC Lupopo, ni mchezaji wa Real Of Kinshasa alijiunga na FC Saint Eloi Lupopo kwa mkopo.

Yanga walishamalizana na klabu yake, FC Lupopo ndio waliochelewesha (ITC) yake.

Note : Tayari klabu ya Yanga imeshaachana na left wing-back wake, Joyce Lomalisa. Boka ndiye mrithi wa Lomalisa.