STARS YAPEWA DRC, ETHIOPIA NA GUINEA KUFUZU AFCON 2025

DROO ya kuwania kufuzu kombe la Mataifa Afrika 2025, AFCON 2025 imefanyika leo Julai 4, 2024 Jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambapo timu za Mataifa 48 yamebaini wapinzani wao kwenye hatua ya makundi kwa toleo la 35 la michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili.

Timu ya taifa ya Tanzania imepangwa kwenye Kundi H sambamba na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Guinea na Ethiopia huku Mabingwa watetezi, Ivory Coast wakipangwa Kundi G sambamba na Zambia, Sierra Leone na Chad.

Wenyeji wa michuano hiyo, Morocco wamepangwa Kundi B sambamba na Gabon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Lesotho.

MAKUNDI

Group A: Tunisia, Madagascar, Comoros, Gambia
Group B: Morocco, Gabon,Central Africa Republic, Lesotho
Group C: Egypt, Cape Verde, Mauritania, Botswana
Group D: Nigeria, Benin Libya, Rwanda
Group E: Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia
Group F: Ghana, Angola, Sudan, Niger
Group G: Cote d’Ivoire, Zambia, Sierra Leone, Chad
Group H: DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia
Group I: Mali, Mozambique, Guinea Bissau, Eswatini
Group J: Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe
Group K: South Africa, Uganda, Congo, South Sudan
Group L: Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi.