RHULAN MOKWENA MAISHA YAKE NDANI YA KIKOSI CHA MAMELODI SUNDOWNS YAMEFIKIA TAMATI

Rhulan Mokwena Maisha yake ndani ya Kikosi Cha Mamelodi Sundowns yamefikia tamati baada ya mabosi wa timu hii tajiri hapa Afrika kuamua kuachana naye wakati huu wapo Kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba wake.

Ugomvi mkubwa wa Rhulan Mokwena na Viongozi wa Mamelodi ni Staili yao ya uchezaji …. Fleming Berg ambaye ni Sporting Director wa timu hii hajawahi kuvutiwa na Soka analo fundisha Rhulan Mokwena pia na falisafa zake za usajili.

Mamelodi Sundowns ni timu tajiri ambayo inaweza kununua mchezaji yoyote yule ikiwa na nyota lukuki lakini imekuwa ikishindwa kupata matokeo mbele ya timu zinazo kaa nyuma muda mwingi.

Fleming Berg alimwambia Rhulan Mokwena mechi za kimataifa hazitaki Mbwembwe nyingi lakini yeye aliamini katika falisafa yake tuu .

Rhulan ameshindwa kutimiza majukumu ya Kimkataba Kwa sababu alitakiwa kutwaa Mataji yote ya Ndani na CAF Champions League..

Kilicho wauma zaidi Mamelodi Sundowns ni kufungwa fainali mara mbili na Orlando Pirates.

Kilicho wakera zaidi Mabosi wa timu hii ni kushindwa kupata bao mbele ya YANGA iliyokosa nyota Kibao muhimu wakati wao Wana amini hii ni timu ya kawaida sana kwao Ndipo Ugomvi wao ulianzia hapa huku kipigo Toka Kwa Esperance Sportive de Tunis kilitoa baraka ya Thank youuu Kwa Rhulan Mokwena.