Timu ya taifa ya Brazil imefuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Mataifa ya Amerika Kusini licha ya kumaliza hatua ya makundi kwa sare ya 1-1 dhidi ya Colombia katika uwanja wa Levi huko Santa Clara, California Marekani.
Brazil imemaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D alama 5 baada ya mechi tatu alama mbili nyuma ya vinara Colombia wenye pointi 7 baada ya mechi 3 ambao pia wamefuzu robo fainali ya Copa America 2024.
Katika mchezo mwingine wa Kundi D, Costa Rica waliomaliza nafasi ya tatu kwa alama nne, imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya washika mkia Paraguay wenye pointi sifuri.
FT: Brazil ?? 1-1 ?? Colombia
⚽ Raphinha 12’
⚽ Munoz 45+2’
Costa Rica ?? 2-1 ?? Paraguay
⚽ Calvo 3’
⚽ Alcocer 7’
⚽ Sosa 55’