RAJA CASABLANCA YA MOROCCO YATWAA UBINGWA KOMBE LA FA THRONE CUP, NABI KAMALIZA KAPA

Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco imetwaa ubingwa kombe la FA Nchini humo (Throne Cup) kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya AS FAR Rabat kwenye fainali. Kipigo hicho kinamfanya kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi kumaliza msimu bila kombe lolote.

FT: AS FAR Rabat 1-2 Raja Casablanca
⚽ Zouhzouh 28’
⚽ Bouzok 6’
⚽ Boulacsou 79’

Hili ni kombe la pili la msimu kwa Raja Casablanca baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Morocco bila kupoteza mchezo wowote.

Raja inakuwa klabu ya kwanza kutwaa makombe mawili ya ndani kwenye msimu mmoja tangu walipofanya hivyo mnamo 1996.