
AZAM YASHUSHA KIUNGO KUTOKA MALI
KLABU ya Azam imefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) kumsajili kiungo mshambuliaji, Franck Tiesse. kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao wa 2024-25. Tiesse (26) anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, akiwa Stade Malien aliisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe…