KIBU DENNIS KIUNGO WA KAZI AIGOMEA STARS

KIUNGO wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda Kibu Denis amekataa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa akidai anakwenda mapumziko nchini Marekani.

Taarifa za uhakika zinasema baada ya kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa na mechi dhidi ya Zambia kwa kuweka kambi ya siku 7 nchini Indonesia, Kibu alikaa kimya hadi siku moja kabla ya kuondoka aliposema anakwenda mapumziko Marekani.

Kibu hajaonekana uwanjani takribani wiki tatu alipokuwa katika majadiliano ya kuongeza mkataba na Simba.

Ipo wazi kuwa kikosi cha Simba ndani ya msimu wa 2023/24 kimegotea nafasi ya tatu baada ya kukusanya jumla ya pointi 69 ndani ya ligi.

Ni mabao 59 timu hiyo imetupia kwa msimu wa 2023/24 huku nyota huyo akifunga bao moja ilikuwa kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.