MITAMBO ya mabao ndani ya Simba imerejea tarayi kwa ajili ya kuendelea kutimiza majukumu ndani ya uwanja baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na sababu mbalimbali. Kwa sasa Ligi Kuu Bara ipo mzunguko wa pili ambapo timu zinakamilisha hesabu bingwa akiwa tayari ameshajulikana ambaye ni Yanga.