MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi wameamua kuja na Gamondi Day kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ikiwa ni mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Mei 22.
Ipo wazi kwamba Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imetwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 27 msimu wa 2023/24.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema: “ukiweza kupiga dongo kama Gamondi wewe piga uje kumpongeza Masta Gamondi. Ametuheshimisha sana, Yanga Bingwa na ushindi mnono wa mabao 7 kwenye Kariakoo Derby.
“Ukiweza kutengeneza picha ya Masta Gamondi, njoo na picha yake uwanjani. Kama unaweza kubeba bango lenye ujumbe wowote njoo nalo. Kwa mfano unaweza kubeba bango limeandikwa Masta Gamondi kiboko wa mayi wetu.”