>

HII HAPA MITAMBO YA MABAO TATU BORA

MSIMU wa 2023/24 unakwenda kugota mwisho kwa kila timu kupambania malengo yake licha ya kwamba tayari bingwa ameshapatikana ambaye ni Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ndani ya tatu bora tayari bingwa ashajulikana ambaye ni Yanga alifanikisha malengo hayo baada ya kucheza mechi 27 akifikisha pointi 71 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ile kwa sasa ndani ya ligi msimu wa 2023/24.

Ni Yanga namba moja kwa wakali kwenye kutengeneza mabao namba moja ni Aziz KI ambaye amehusika kwenye jumla ya mabao 23 kati ya 60 yaliyofungwa na timu hiyo inayonolewa na Gamondi.

Aziz KI kafunga jumla ya mabao 15 akitumia mguu wa kushoto kufunga mabao 13 na ule wa kulia akifunga mabao mawili huku akitoa jumla ya pasi 8 zilizoleta mabao kwenye timu hiyo.

Feisal Salum wa Azam FC iliyo nafasi mbili kwenye ligi baada ya mechi 27 ikiwa na pointi 60 yeye kahusika kwenye mabao 22 kati ya 54 yaliyofungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu,Yusuph Dabo.

Fei kafunga mabao 15 kibindoni akiwa katengeneza jumla ya pasi 7 za mabao ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC baada ya kujiunga nao akitokea kikosi cha Yanga.

Ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda baada ya kucheza mechi 27 na kukusanya mabao 52 nafasi ya tatu mkali wa kutengeneza mabao ni Clatous Chama.

Chama amehusika kwenye mabao 13 ndani ya Simba akifunga mabao 7 na kutengeneza jumla ya pasi sita za mabao ndani ya timu hiyo ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo.