YANGA V AZAM FC FAINALI

YANGA imetinga hatua ya fainali ya CRDB Federation Cup kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ni dakika ya 104 bao la ushindi kwa Yanga limefungwa na Aziz KI katika mchezo wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Ni fainali ya nne kwa Yanga katika CRDB Federation Cup wanakwenda kukutana na Azam FC, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Manyara.

Itakuwa ni fainali dhidi ya Azam FC iliyopishana na taji hilo msimu uliopita kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga bao la Kenedy Musonda.