MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa YangaYanga amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ihefu unaotarajiwaunaotarajiwa kuchezwa leo Mei 19 2024 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
YangaYanga ni mabingwa watetezi wa CRDB Federation Cup walitwaa taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0 Azam FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Tayari Azam FC imetinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Gamondi amesema: “Tunatambua utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari kwa kuwa wachezaji wanapenda kushinda na wamekuwa wakifunga hilo lipo wazi ukitazama hata mashindano yetu wapo kwenye chati ya ufungaji.”.
Kinara wa utapiaji ndani ya CRDB Federation Cup ni Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga ambaye amefunga jumla ya mabao matano.