YANGA YATUMA UJUMBE HUU IHEFU

KUELEKEA kwenye mchezo wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup mabingwa watetezi wa taji hilo Yanga wamebainisha kwamba hesabu kubwa ni kufanya vizuri kwa kupata matokeo chanya.

Yanga inakutana na Ihefu Mei 19 Uwanja wa CCM Kirumba kwenye nusu fainali ambapo mshindi atakutana na Azam FC kwenye fainali iliyopata ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema: “Tunaamini tuna kila sababu ya kuendelea kufanya vizuri msimu huu, tuna wachezaji wanaopenda kutafuta magoli na kufunga ndio maana wachezaji wetu wapo kwenye orodha ya wafungaji bora kwenye kila mashindano.”

Kwa upande wa beki wa kazi Dickson Job amesema: “Tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho na benchi la ufundi chini Kocha wetu Gamondi wameshamaliza kutupa maelekezo yote ni sisi kwenda kuipambania Klabu yetu na kuibuka na ushindi kesho.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba Mashabiki wetu wote wa Arusha na mikoa ya jirani kuja kwa wingi kesho kutupa sapoti.”