MABINGWA watetezi wa taji la CRDB Federation Cup wana kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Ihefu katika mchezo wa hatua ya nusu fainali, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi, Yanga ilianza raundi ya pili kwa kushuhudia ubao ukisoma Yanga 5-1 Hausing, Yanga 5-0 Polisi Tanzania, Dodoma Jiji 0-2 Yanga raundi ya nne na robo fainali ilikuwa Yanga 3-0 Tabora United.
Ni mabao 15 safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga na kinara akiwa nj Clement Mzize mwenye mabao 5 huku ukuta ukiruhusu bao moja pekee ndani ya dakika 360.
Nusu fainali itakuwa dhidi ya Ihefu Mei 19 ambapo Ihefu wao ilikuwa Ihefu 3-0 Rospa FC raundj ya pili, Ihefu 2-0 Mbuni, KMC 0-3 Ihefu, Ihefu 0-0 Mashujaa ile ya Kigoma, ikashinda kwa penalti 4-3.
Ni mabao 8 safu ya ushambuliaji ya Ihefu imefunga na ukuta haujaruhusu bao la kufungwa ndani ya dakika 360.