LIGI KUU BARA: DODOMA JIJI 0-1 SIMBA

FT: LIGI Kuu Bara

Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Dodoma Jiji 0-1 Simba

Goal Michael Fred dakika ya 7

DODOMA Jiji wapo nyumbani Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakisaka pointi tatu mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda.

Simba ikiwa ugenini nayo hesabu zake ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo ambao una ushindani mkubwa.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.

Hivyo Dodoma Jiji wanasaka kutibua rekodi ya mzunguko wa kwanza kupishana na pointi na Simba hesabu ni kuvuna pointi nyingine.