DEAR MSOMI KAZI KALI KUTOKA KWA NYASUBI

DEAR msomi ni zawadi ya mwamba Nacha A Sound From Nyasubi anakwambia mafanikio na elimu haviusiani unajikuta unajikuta dalali na ulisomea urubani, nyumbani huwezi kaa sio vimbetwa.

Kazi kubwa ya ubongo wa mwamba anayefanya vema katika muziki wa kizazi kipya akiwa na mkali kutoka Morogoro Stamina halafu kiitikio ni sauti ya Mkwawa.

Stamina anasema shepu your mind akili kama huna huna huwezi kuichubua akili…

Video imekaa poa sana, director kacheza na mwanga pamoja na shoot ambazo haziboi kuitazama.

Ile Stamina anasema eti mtu ana degree ya ufugaji anaishia kufuga ndevu..

Moja ya kazi nzuri ambazo zimeandikwa na kutoka kwenye mikono ya mkali Nacha ambaye hana jambo dogo kwenye utunzi.

Anayajua mashairi na anajua kwenda na mwendo katika kuimba taratibu hachoshi kusikilizwa kila la kheri Nacha na maisha mema.