BBD AFUNGUKIA ISHU YA UBINGWA YANGA

YANGA baada ya kucheza mechi 27 safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 60 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zake kibindoni ni 71.

Kinara wa mabao ndani ya Yanga ni Aziz KI ambaye katupia jumla ya mabao 15 na pasi 8 za mabao.

KI amehusika katika mabao 23 yaliyofungwa na Yanga ambao ni mabingwa msimu wa 2023/24.

Big Brain Defender, (BBD) beki wa kupanda na kushuka Dickson Job amefungukia ishu ya Yanga kutwaa ubingwa akiweka wazi kuwa ulikuwa ni mpango kazi wa muda mrefu kuvuna pointi tatu kwenye mechi ambazo wanacheza.

“Kikubwa kwenye kila mchezo ilikuwa tunahitaji pointi tatu na hilo limewezekana kutokana na ushirikiano ambao unaendelea ndani ya timu na benchi la ufundi.”

Job mwamba ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya ligi alifunga katika mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja Azam Complex.