>

SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA KAITABA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa walikuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar nafasi hawakuzitumia.

Ubao wa Uwanja wa Kaitaba umesoma Kagera Sugar 1-1 Simba baada ya dakika 90 ambapo Simba walianza kufunga kwenye mchezo wa leo.

Ladack Chasambi alifungua akaunti ya mabao dakika ya 24 lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo wachezaji wa Simba walifanya makosa yaliyotumiwa na Kagera Sugar,

Obrey Chirwa alimtungua Ayoub Lakred ambaye alianza langoni kwenye mchezo wa leo mwisho wakagawana pointi mojamoja Simba ikifikisha pointi 57 nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Mgunda amesema: “Tulikuwa na nafasi ya kupata matokeo, tumetengeneza nafasi nyingi lakini hatujazitumia hivyo makosa tutafanyia kazi.”