MWAMBA Mudathir Yahya ndani ya Ligi Kuu Bara ana balaa zito kutokana na kazi anayofanya katika kutimiza majukumu yake akishirikiana na wachezaji wengine.
Alipokuwa huru alikuwa akitajwa kuhitajika ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuachana na mabosi wake Azam FC ambao walieleza kuwa walifikia hatua ya kuachana na nyota huyo kwa kuwa hakuwa tayari kuongeza mkataba mpaka pale atakapopata ushauri.
Simba walikuwa wanatajwa kuisaka saini yake lakini walipishana naye kwa kinachotajwa kuwa ni hofu ya kiwango chake kuporomoka kwa sababu hakucheza muda mrefu.
Muda sasa gari limeweka akionyesha uwezo wake ndani ya uwanja, mabao 9 kibindoni msimu wa 2023/24.
Katika mabao hayo sita kafunga Uwanja wa Azam Complex msimu wa 2023/24 ambapo Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 68 kibindoni.