KIKOSI cha Simba leo Mei 12 kinakazi ya kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita kwa Simba ilikuwa ni Mzizima Dabi, Mei 9 2024 walishuhudia ubao ukisoma Azam FC 0-3 Simba.
Inakutana na Kagera Sugar inayocheza mpira wa kasi na kujilinda kwa nguvu ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua Uwanja wa Kaitaba ni mgumu na mchezo utakuwa mgumu lakini wanahitaji pointi tatu muhimu.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu mashabiki wajitokeze kwa wigi.”
Watakosa huduma ya kiungo mshambuliaji Clatous Chama, Kibu Dennis huku Shomari Kapombe kukiwa na hatihati ya kuanza licha ya kurejea katika uwanja wa mazoezi.