VITA ndani ya tano bora ni kali msimu wa 2023/24 kwa kila timu kupambania pointi tatu ndani ya dakika 90 kufikia malengo yao.
Ikumbukwe kwamba Mei 10 2024 vumbi kwenye ligi iliendelea huku Coastal Unio wakionyesha ubabe mbele ya wakali kutoka Singida, Singida Fountain Gate ambao kwa sasa makazi yao yapo Mwanza.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, umesoma Coastal Union 2-0 Singida Fountain Gate ikiwa ni mzunguko wa pili wenye ushindani mkubwa kwa timu zote.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Crispin Ngushi dakika ya 26 na Greyson Gwalala dakika ya 46, pointi 37 nafasi ya nne kwa Coastal huku Singida Fountain Gate pointi 29 nafasi ya 11.
Mchezo mwingine uliochezwa ilikuwa wababe wawili Dodoma Jiji dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo kila timu ilikuwa kazini kusaka pointi tatu.
Baada ya dakika 90 wote waligawana pointi mojamoja kwa kutoshana nguvu bila kufungana.