Skip to content
NYOTA wa Azam FC, Feisal Salum amebainisha kuwa watarejea uwanjani wakiwa imara zaidi licha ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Simba.
Ipo wazi kwamba kwenye Mzizima Dabi mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 9 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-3 Simba.
Kiungo Fei Toto kwenye mchezo huo alikosa penalti baada ya pigo lake la mpira kugonga mwamba dakika ya 33 ikiwa ni salama kwa kipa Ayoub Lakred.
Nyota huyo mwenye mabao 15 kwenye ligi na pasi 7 za mabao ameweka wazi kuwa watapambana kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata.
“Ilikuwa mpango mkubwa kupata pointi tatu bahati mbaya tukakosa matokeo hivyo bado tuna nafasi yakufanya vizuri kwa mechi ambazo zimebaki.
“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani kazi bado inaendelea na tuna nafasi ya kupata matokeo tutarejea uwanjani tukiwa imara zaidi,”.