AZAM FC WATOA TAMKO HILI ISHU YA KUPOTEZA MBELE YA SIMBA

UONGOZI wa Azam FC umebainisha kuwa walishindwa kutumia nafasi ambazo walipata katika Mzizima Dabi dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 9 2024.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-3 Simba na pointi tatu zikaelekea Msimbazi.

Katika mchezo huo kiungo mshambuliaji Feisal Salum alikosa pigo la penalti dakika ya 33 baada ya Che Malone kumchezea faulo nyota wa Azam FC Gibril Sillah.

Dakika ya 69, Azam FC walipata bao kupitia kwa Nado mwamuzi msaidizi alibainisha kuwa mfungaji alikuwa katika mtego wa kuotea.

Thabit Zakaria, Meneja wa Idara ya Habari Simba amesema: “Tulipata nafasi ikiwa ni pamoja na penalti aliyotupa mwamuzi Ahmed Arajiga lakini tukakosa ni sehemu ya mchezo.

“Lakini pia mwamuzi msaidizi alitunyima bao ambalo tulifunga kwa kuwa mfungaji hakuwa katika eneo la kuotea,”.

Azam FC kwenye msimamo wa ligi ni namba mbili baada ya kucheza mechi 26 imekusanya pointi 57 Simba nafasi ya tatu na pointi zake ni 56 ikiwa imecheza mechi 25.