KIUNGO wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Jonas Mkude maarufu kwa jina la Nungunungu amepenya kwenye orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora ndani ya kikosi hicho.
Mkude amekuwa katika ubora wake hivi karibuni baada ya kupewa nafasi kucheza katika mechi za ushindani alikuwa kwenye kikosi cha Yanga kilichokomba pointi tatu dhidi ya watani zao wa jadi Simba.
Katika mchezo huo uliochezwa Aprili 20 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba. Mabao yalifungwa na Aziz KI na Joseph Guede kwa upande wa Yanga.
Bao la Simba lilifungwa na Michael Fred likiwa ni bao pekee la kufutia machozi kwenye mchezo huo.
Wachezaji wengine ambao wamepenya kwenye kuwania tuzo hiyo inayodhaminiwa na NIC Insurance ni Djigui Diarra na Guede kwa Aprili.