SIMBA YAMTANGAZA WAZIRI WA MAJI MGENI RASMI DHIDI AL AHLY LEO

Klabu ya Simba imemtangaza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly utakaochezwa leo Machi 29, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 3 usiku.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Simba ambao wanahitaji matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.