SIMBA; MASHABIKI KUFIKA UWANJANI NI MATENDO YA LAZIMA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa miongoni mwa matendo ya lazima kwa mashabiki wa Simba ambao wana afya njema na mapenzi na timu hiyo ni kufika uwanjani Machi 29 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa hatua ya robo fainali ambapo mashabiki wameendelea kununua tiketi kwa ajili ya kuwa sehemu ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amebainisha kuwa nguvu kubwa ya kupata ushindi inaongezewa chachu na uwepo wa mashabiki hivyo ni muhimu kujitokeza uwanja wa Mkapa.

“Miongoni mwa matendo ambayo ni ya lazima kwa mashabiki wa Simba ni kujitokeza Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wetu wa kimataifa kwa kuwa tunaamini utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa tupo tayari.

“Tumekuwa na wakati mwingi wa maandalizi na baada ya kufika hatua ya robo fainali kila kitu kimebadilika kuanzia mipango na ari sasa hao wapinzani wetu Al Ahly Uwanja wa Mkapa hamna namna tutamalizana nao mapema kwa kuhakikisha kazi inaishia hapa na mashabiki wana nguvu kubwa kwenye hili.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi itakuwa ni fainali ya kipekee kwelikweli na watafurahi namna wachezaji watakavyotoa burudani kwenye mchezo wetu tukiwa nyumbani na tunakwenda kukamilisha kazi ugenini tukiwa na nguvu mpya,”