BEKI WA KAZI YANGA AKIRI UGUMU WANAOPATA

BEKI wa Yanga, Gift Fred amebainisha kuwa kazi ni ngumu kwenye mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na ushindani wanaopata kutoka kwa wapinzani wao uwanjani.

Fred bado hajawa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kwenye mechi ambazo anapewa nafasi miguu yake haikuwa na ajizi katika kutimiza majukumu yake.

Ikumbukwe kwamba miongoni mwa mchezo ambao alipata nafasi ya kucheza ilikuwa dhidi ya Mashujaa Uwanja wa Azam Complex Yanga iliposhinda 1-0.

Beki huyo amesema kuwa kila mchezo ambao wanacheza ni muhimu kupata matokeo jambo ambalo linawafanya waongeze umakini na kutimiza majukumu kwa ushirikiano.

“Kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza ushindani ni mkubwa na kilatimu inajitahidi kufanya vizuri kutafuta matokeo ambacho sisi tunakifanya ni kuongeza umakini.

“Furaha yetu ni kuona kwamba hatupotezi mechi na hilo linawezekana kwa kuwa tunacheza tukiwa ni timu licha ya wapinzani wetu nao kuwa na ubora, ambacho kinatokea tukipata nafasi tunazitumia na kwetu upande wa ulinzi haturuhusu kufungwa,”.