YANGA: TUTAPAMBANA MPAKA TONE LA MWISHO

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa watapambana mpaka tone la mwisho kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikumbukwe kwamba Yanga katika mzunguko wa kwanza ilipoteza mchezo mmoja pekee ugenini kwa kuhushudia ubao wa Uwanja wa Highland Estate ukisoma Ihefu 2-1 Yanga na mzunguko wa pili walilipa kisasi kwa ushindi wa mabao 5-0.

Mzunguko wa pili ni mchezo mmoja walipoteza dhidi ya Azam FC ubao ulisoma Azam FC 2-1 Yanga na bao la ushindi lilfungwa na Feisal Salum dakika ya 52.

Kocha huyo amesema kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi jambo ambalo linawafanya wafanye maandalizi mazuri kwenye kila mchezo wanaoshuka uwanjani.

“Ratiba ni ngumu kwenye mechi ambazo tunacheza hilo tunalitambua lakini sisi tunayo njaa ya kupata pointi tatu kwenye mechi ambazo zipo mbele yetu kwa kuwa muhimu ni kupata ushindi.

“Hizi mechi ambazo tunacheza ni muhimu kupata ushindi kuwa kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi.Natambua kwamba wachezaji wangu wanapitia kwenye nyakati ngumu kutokana na uchovu lakini tutapigana mpaka tone la mwisho,”