>

TAIFA STARS KAMILI KIMATAIFA, HALI YA HEWE TATIZO

KOCHA wa Timu ya Taifaya Tanzania, Taifa Stars, Hemedi Sulemaini amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mechi zinazowakabili licha ya hali ya hewa kuwa ngumu kidogo watazoea taratibu.

Kocha huyo amebainisha kwamba taratibu wanaendelea kuwa kwenye mfumo kutokana na maandalizi ambayo wanafanya na imani ni kufanya vizuri kwenye mechi zao zote.

Taifa Stars walifanya mazoezi Uwanja wa Olimpiki wa Baku, Azerbaijan kujiandaa na michezo miwili ya FIFA Series 2024.

Kocha huyo amesema: “Tunamshukuru Mungu tumefika salama na kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni maandalizi kuelekea mechi zetu zote licha ya ugumu kidogo kwenye hali ya hewa kwa kuwa ipo tofauti na Dar.

“Hakuna namna wanajitahidi kuizoea kwa sababu hata mechi zetu tutacheza kwenye hali ya hewa ya namna hivyo ni wakati wa kuendelea kufanya maandalizi zaidi,”..

Miongoni mwa wachezaji waliopo na timu ya taifa ya Tanzania ni Mohamed Hussein, Feisal Salum, Clement Mzize, Aishi Manula.