MSIMU wa 2023/24 unaingia kwenye orodha ya msimu ambao Simba inapitia magumu kutokana na mwendo wake kutokuwa bora ndani ya uwanja katika mechi za ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara. Kwa upande wa rekodi kwa timu na namba binafsi kwa wachezaji wanaotimiza majukumu kikosi cha Simba kwa hivi karibuni haujawa kwenye ubora ambao ulikuwa unatarajiwa ikiwa inapambania kufikia malengo yake.
Baada ya mechi 19 ni mchezaji mmoja pekee ambaye anaingia ndani ya tano bora katika rekodi binafsi tofauti na 2022/23 ambapo walikuwa wakipambana kufanya vizuri ambapo Clatous Chama alikuwa kwenye ubora wake katika pasi za mwisho.
Msimu wa 2023/24 hajawa na mwendo mzuri lakini bado anaingia kwenye tano bora ya wachezaji wenye pasi nyingi akiwa ametoa jumla ya pasi zake tano za mabao ndani ya ligi.
Kwenye ufungaji tatizo kinara ni Saido Ntibanzokiza mwenye mabao 7 msimu wa 2022/23 alitupia mabao 17, ulinzi tatizo ndani ya tatu bora Simba ni namba moja kwenye kufungwa mabao mengi ambayo ni 18.
Timu hiyo kwa sasa ipo Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.