BAADA ya Hemed Morocco kutangaza orodha ya wachezaji watakaokuwa katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, safari imeanza kwa ajili ya kuelekea Azerbaijan ambapo wanatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki.
Tayari kikosi cha Taifa Stars kimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul, Uturuki muda wowote kitakwe pipa kuelekea Baku, Azerbaijan kwenye mashindano ya FIFA Series.
Wakiwa nchini humo Stars watacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Bulgaria na Mongolia.