WAKATI wakitarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye msako wa pointi tatu muhimu mkali wa Mzizizma Dabi ni Aziz KI.
Aziz KI kahusika kwenye mabao 19 kati ya 48 yaliyofungwa na Yanga akiwa kafunga 13 na kutengeneza pasi za mabao 6 msimu wa 2023/24 kwenye ligi.
Ni yeye mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC alifunga hat trick ikiwa ni rekodi ndani ya Mzizima Dabi.
Machi 17 Uwanja wa Mkapa Azam FC v Yanga Saa 2:15 ambapo kila timu imebainisha kwamba ipo tayari kwa mchezo huo.